Kesi mbili zimewasilishwa katika mahakama ya juu nchini Kenya, zikitaka kufutwa kwa ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kufuatia uchaguzi wa tarehe 26 mwezi Oktoba.
Kesi hizo ziliwasilisha mahakamani Jumatatu saa chache kabala ya siku ya mwisho.
Aliyekuwa mbunge wa kilome Harun Mwau na mawakili Njonjo Mue na Khelef Khalifa, wanasema kuwa katiba ilikiukwa wakati wa maandalizi ya uchaguzi huo.
Mwau alijumuisha kipengee cha uamuzi wa mahakama, kuwa mgombea kwa chama cha United Democratic Cyrus Jirongo alikuwa amefilisika kwa hivyo hakustahili kuwania urais.
Kesi iliyowasilishwa na mawakili Mue na Khalifa nayo kwa upande mwngine ilizunguzia ukiukaji wa katiba ikiwemo kuchapisha picha za watu wasiostahili kwenye makaratasi ya urais akiwemo mgombea wa muungano wa NASA Raila Odinga, ambaye alikuwa ametangaza kuwa hangegombea urais.
Akiongea na vyombo vya habari wakati wa kuandika kesi hiyo, wakili wa Mue na Khalifa, Harun Ndubi, alisema kwa tume ya uchaguzi haukustahili kuandaa uchaguzi kwa hivyo wanataka uchaguzi huo kuandaliwa upya.
Ndubi alisema kuwa tume ya uchaguzi ilikuwa na upendeleo kwa hivyo haikustahili kuandaa uchaguzi.
Ndubi aliwaambia waandishi wa habari kuwa kumjumuisha Odinga kwenye makaratasi ya kura licha ya yeye kujiondoa kuliwachanganya wapiga kura.
/ BBC SWAHILI

No comments :
Post a Comment