airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, November 16, 2017

Kiongozi wa Vijana Zanu-PF ajishusha Aomba Jeshi Msamaha!

Kiongozi wa muungano wa vijana wa chama tawala Zanu-PF Kudzai Chipanga, ambaye amekuwa muungani mkono wa Rais Robert Mugabe na mkewe Grace ameomba radhi kutokana na hatua yake ya kulishutumu na kulionya jeshi dhidi ya kuchukua mamlaka nchini humo.

Jumanne, alikuwa amemwambia mkuu wa majeshi Jen Constantino Chiwenga anafaa “kusalia kwenye kambi za jeshi”.

Alisema wanachama wake hawatakubali wanajeshi wakiuke katiba na kwamba yeye na wafuasi wake walikuwa tayari kufariki wakimtetea Mugabe.Lakini usiku wa kuamkia leo, alisoma taarifa kwenye runinga ya taifa ZBC, akisema kwamba alikuwa amekosea.

Tangu wakati huo nimetafakari na kutambua binafsi kwamba nilikosea, pamoja na wakuu wenzangu kwa kudunisha afisi yako yenye heshima.

Sisi bado ni wadogo na hufanya makossa na tumejifunza mengi kutokana na makosa haya.

No comments :

Post a Comment