dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 29, 2017

Maaskofu wafunguka kwa Rais Kabila!

Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamemtaka Rais Joseph Kabila kujitokeza hadharani na kutangaza kuwa hatagombea urais kwa muhula wa tatu.
Kauli hiyo ya Maaskofu imekuja baada ya mkutano wao kuthamini hali ya kisiasa nchini humo huku kukiwa na na shinikizo kutoka Jumuiya ya Kimataifa, kwa serikali ya DRC kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kama ilivyopangwa.
Hata hivyp hayo yanajiri wakati ambapo serikali ya DRC imepiga marufuku maandamano yaliyopangwa wiki hii kushinikiza kujiuzulu kwa Rais Joseph Kabila.

Uchaguzi Mkuu nchini DRC umepangwa kufanyika nchini humo mwezi Disemba mwakani wakati huo upinzani wa nchi hiyo umekuwa ukidai kuwa  Kabila anapanga kuwania tena kinyume cha katiba, madai ambayo Rais huyo bado hajajibu.

No comments :

Post a Comment