dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, November 20, 2017

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA KUPINGA USHINDI WA KENYATTA...SASA KUAPISHWA KUWA RAIS!



Mahakama ya Juu nchini Kenya imetupilia mbali kesi zilizofunguliwa na wafuasi wa NASA za kupinga ushindi wa Urais wa Uhuru Kenyatta, kwenye uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26, 2017.

Kesi hiyo ambayo ilikuwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari, iliongozwa na majaji 6 akiwemo Jaji Mkuu David Maraga, na kutoa uamuzi kuwa Uhuru Kenyatta ni mshindi halali wa uchaguzi wa Oktoba 26.

Kufuatia uamuzi huo wa mahakama ya Juu nchini Kenya, Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa wiki ijayo, na kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa muhula wa pili.

Ikumbukwe uchaguzi wa marudio ulifanyika baada ya Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya Urais ya uchaguzi wa kwanza wa Agosti 8, 2017 na kutaka urudiwe mara ya pili.

Tume ya Uchaguzi imefurahia uamuzi wa Mahakama ya Juu na kusema ni dhihirisho la kujitolea kwa tume hiyo kufanikisha uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika.

Imesema kupitia taarifa kwamba inasubiri uamuzi wa kina ambao utaiongoza katika kutathmini uchaguzi huo ulivyokuwa pamoja na mipango yake ya kuimarisha uchaguzi na tume yenyewe.

No comments :

Post a Comment