zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 7, 2017

Mashinji afunguka viongozi wa Chadema kukamatwa!

Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, Dkt. Vicent Mashinji amefunguka na kuweka wazi  kwamba kuna mpango wa Wabunge wa chama chake kukamatwa.

Dkt. Mashinji ametumia ukurasa wake wa Twitter usiku wa kuamkia leo kutoa taarifa hiyo ambapo pia ameweka wazi kutokana na mipango hiyo Chama chao kipo imara kuhakikisha wanafikia malengo katika uchaguzi unaoendelea.

"Kuna mpango wa kukamata wabunge walau 5 wakati huu wa kampeni. CDM ipo imara kuhakikisha inafikia malengo ya uchaguzi huu. Haki huleta Amani" Dkt. Mashinji.Aidha Jumapili ya mwisho wa wiki hii Mbunge wa Arusha Godbless Lema aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba "Mkakati umepangwa,nikamatwe na  na Jeshi la Polisi leo, (Siku ya Jumapili) maelekezo yamekwishatolewa . Tunaishi maisha magumu sana, hatuna budi kuvumilia"



No comments :

Post a Comment