dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, November 16, 2017

Tunahitaji serikali ya mpito - Joice Mujuru!

Joice Mujuru, makamu wa rais wa zamani na kiongozi wa muungano wa upinzani wa People's Rainbow Coalition (PRC), ameomba kuwepo na mazungumzo yanayoshirikisha wahusika wote nchini humo.

Amesema matokeo ya mazungumzo hayo inafaa kuwa uchaguzi huru na wa haki Zimbabwe.

Amani inaweza tu kupatikana kwa kuvumiliana na kubadilishana mawazo kwa Wazimbabwe wenyewe. Tukisonga mbele … matukio ya kisiasa yanahitaji kuhusisha wadau wote muhimu humu nchini.Shughuli ya kujenga upya nchi yetu na kuhakikisha maridhiano ya taifa inaweza tu kutokea iwapo kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki, ambao utafanyika kwa kipindi kifaacho na kitakachoafikiwa wakati wa kuunda serikali ya mpito.

Kabla ya kufutwa kazi kwake mwaka 2014, Bi Mujuru alitazamwa na wengi kama mrithi mtarajiwa wa Bw Mugabe.

Hata hivyo alifukuzwa kutoka kwenye chama tawala mwaka 2015.

Mwezi uliopita, alichaguliwa kuwa kiongozi wa muungano wa vyama sita vya upinzani kwa jina People's Rainbow Coalition.

No comments :

Post a Comment