dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 15, 2017

Vitisho vyaendelea kumuandama Nyarandu!

Ndg, Lazaro Nyalandu
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini. Mh. Lazaro Nyalandu ameomba kuombewa yeye pamoja na familia yake kwa kudai kwamba  amekuwa akipokea vitisho visivyo na idadi baada ya kuondoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Usiku wa kuamkia leo Nyalandu ametumia ukurasa wake wa twittter ambao ameonyesha hofu yake na kudai kwamba njia zote zinatumika kuhakikisha ananyamazishwa."Napokea  idadi isiyo ya kawaida ya vitisho tangu kuondoka CCM chama cha tawala. Ni ajabu kuwa kuna hofu kubwa kutoka kwa wasomi, ambao wanatumia njia zote zinazowezekana kuninyamazisha" Nyalandu

Ameongeza "Tafadhali niombeeni mimi pamoja na familia yangu wakati wa majaribu haya tunayopitia".

Kabla ya kuhamia Chadema mapema mwanzoni mwa mwaka huu, Nyalandu alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM.

No comments :

Post a Comment