dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, November 20, 2017

ZANZIBAR: UZEMBE WA HALI YA JUU WATOKEA KWENYE ICU YA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA, ZANZIBAR!

Above: Zanzibar's main referral hospital - Mnazi Mmoja Hospital!

ZANZIBAR: Mgonjwa ambae alilazwa kwenye chumba cha ICU katika hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja, akipatiwa intensive emergency care kutokana na kuwa hali yake ilikuwa mbaya sana, ilionekana asubuhi ya Jumaatatu tarehe 20 November kuwa oxygen iliyokuwa ikimsaidia ilikuwa imekwisha zamani bila ya wahudumu wa hicho chumba cha ICU kutambua. Haijulikani hio oxygen ilikwisha kuanzia wakati gani nyuma. 

Baada ya kufahamika kuwa oxygen ilikwisha wahusika wakaanza mbio mbio kumfanyia mechanical pumping mpaka oxygen ilipopatikana tena, lakini ilikuwa too late na haikuchukuwa muda mkubwa baada ya hapo mgonjwa akafariki.

Waliogunduwa kuwa oxygen ilikwisha walikuwa ni jamaa wa mgonjwa ambao ni wajuzi wa mambo ya tiba waliokuenda kumjulia hali asubuhi na wakamuona mgonjwa wao kapiga rangi ya kijani mikononi na miguuni na walivyoangalia gesi ya oxygen wakaiona imekwisha bila ya nurse kujua. Inaonesha nurse usiku kucha alikuwa kajilalia bila ya kumpitia mgonjwa na kujua hali yake.

Wenye ndugu yao aliefariki wanaishutumu hospitali ya Mnazi mmoja kwa uzembe huu na kuwa ndugu yao ameuliwa na wafanyakazi wa hospitali hii kutokana na kushindwa kwao kufanya kazi zao kama wanavyotakiwa.

Jitihada hazikufuzu za kumtafuta kwa simu Waziri wa Afya wa Zanzibar ambae yupo Toronto, Canada, ili aulizwe vipi mgonjwa anaepelekwa kwenye ICU kwenye main referral hospital kama ya Mnazi Mmoja ambayo ndio ya juu kabisa Visiwani na baadae anakosa maangalizi ya 24/7 kama inavyotakiwa kwa mgonjwa anaelazwa kwenye ICU. 

1 comment :

  1. Duu.
    Hii ni hatari.
    Huyo nurse bado hajafukuzwa kazi?
    Kufukuzwa kazi haitotosha, bali apelekwe mahakamani akajibu masuala ya hii criminal case yake.

    ReplyDelete