Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi (SACP), Wilbroad Mutafungwa amesema mtoto huyo inadaiwa aliuwawa na kutumbukizwa kwenye kisima cha maji katika kijiji cha Budushi kata ya Ndala wilayani Nzega Mkoani Tabora.
"Ni kweli tulipokea taarifa za tukio hilo la mtoto kukutwa katika kisima cha maji na baadae kuzikwa, tuliamua kwenda mahakamani kuomba hati ya kufukua maiti ili tufanye uchunguzi, baba mzazi wa mtoto huyo bado tunamshikila kwa ajili ya upelelezi", amesema Kamanda Mutafungwa.
Sambamba na hilo Kamanda Mutafugwa amewaomba wananchi wawe wavumilivu katika kipindi hiki ambacho Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi, ili kubaini chanzo zaidi cha mtoto huyo kufariki, na mara utakapokamilika watatoa taarifa zaidi ya tukio hilo.
No comments :
Post a Comment