dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 1, 2017

MASAUNI AFUNGUA MKUTANO WA UCHAGUZI WA JUMUIYA YA UMOJA WA WAZAZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA DAR ES SALAAM!


Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa chama hicho, mkoa wa Dar es Salaam, mkutano huo umefanyika leo, katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha Wetu

Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam, Angela Kizigha, akizungumza wakati wa Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa chama hicho, mkoa wa Dar es Salaam. Kushoto aliyevaa kofia ni Mgeni Rasmi na Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni. Mkutano huo umefanyika leo, katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam. 

Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi cheti cha Uongozi , Kiongozi anayemaliza muda wake katika Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam, Ibrahim Mpwapwa (kulia), wakati wa mkutano uliofanyika leo,ukumbi wa Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam

Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akipiga makofi baada ya kuwasili katika Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa chama hicho,mkoa wa Dar es Salaam, Mkutano huo umefanyika leo Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam

Wajumbe wa Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi,mkoa wa Dar es Salaam, wakishangilia wakati Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), akizungumza katika mkutano huo uliofanyika leo, ukumbi wa Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam

No comments :

Post a Comment