dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 3, 2017

Mtulia awataka wananchi wachague CCM uchaguzi ujao!


Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Maulid Said Abdallah Mtulia amewataka wananchi wa wilaya ya Kinondoni kuchagua Mbunge wa Chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi ujao ili kuharakisha maendeleo katika jimbo.

Mhe. Mtulia ambaye jana tarehe 2 Novemba, 2017, alitangaza kujivua uanachama wa CUF na nafasi zake zote za uongozi ndani ya Chama hicho amesema wananchi endapo watamchagua Mbunge kutoka Chama tawala basi maendeleo yatakuja kwa haraka kuliko Mbunge anayetoka vyama vya upinzani.

“Naamini Kama ningekuwa Mbunge wa Chama tawala ningeweza kutekeleza vizuri zaidi ahadi zangu ambazo nimezitoa kwa wananchi wangu.. Kwa sababu hiyo nimeona sasa ni bora nijivue nafasi zangu zote (Ndani ya CUF) na kama uchaguzi ukifanyika wananchi wa Kinondoni wasifanye makosa wahakikishe wanamchagua Mbunge anayetokana na Chama tawala ili awe kiunganishi kati yao na serikali yao waweze kupata maendeleo kwa haraka zaidi.“amesema Mhe. Mtulia.

No comments :

Post a Comment