dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 1, 2017

Nyalandu afunguka kinachoendelea Libya!

Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa wa Singida Kaskazini aliyejiuzulu, Lazaro Nyalandu ameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua zaidi juu ya kinachoendelea nchini Libya.

Mh. Nyalandu amesema kwamba ni lazima hatua zichukuliwe kwa kile kinachoendelea nchini Libya kwa vile  kinachoshuhudiwa kwa sasa ni matusi kwa wanadamu.

Kupitia kwenye mtandao wake wa Twitter Mh. Nyalandu ameandika

"Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika lazima uchukue hatua dhidi ya Libya sasa.Tunachoshuhudia ni matusi kwa wanadamu" Nyalandu

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa zikiripotiwa kutoka Libya kwamba kumekuwa na biashara ya utumwa ikifanyika ikihusisha Libya kuuza waafrika wengine nchi za Ulaya.

Siku ya jana Ubalozi wa Libya nchini Tanzani umesema Waafrika wanaosemwa wanauzwa kutoka Libya, yawezekana walikuwa wanakabidhiwa kwa watoroshaji ili wawapeleke Ulaya na sio kuwauza kama watumwa.




No comments :

Post a Comment