dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 1, 2017

USIKU WA KUPENDEZA WITH DR. SHIKA IN TORONTO, CANADA!

BILIONEA DR SHIKA KWENYE MNADA AKIZUNGUKWA NA WATU WANAOMHUSUDU!
 BILIONEA DR SHIKA NI MPENZI WA WOTE
 DR SHIKA NI MCHEZAJI MPIRA MZURI SANA
 DR. SHIKA AKIONEKANA KWENYE OFFICIAL FUNCTION MOJA MJINI DAR ES SALAAM HIVI MAJUZI

ZANZIBAR. Habari zilizotufikia kutoka Toronto, Canada zinasema kuwa yule bilionea alietaka kununua nyumba za Lugumi  mjini Dar Es Salaam, lakini akashindwa kutoa 25% ya bei za nyumba hizo baada ya mnada kumalizika, atatembelea jiji la Toronto, Canada hivi karibuni na kuzungumza na Watanzania wa huko.

Inasemekana kuwa mipango inapangwa huko Toronto, Canada ili Dr. Shika aitembelee nchi hio hivi karibuni. 

Mpaka sasa hivi haijulikani kama Dr Shika ameukubali mualiko huo, lakini vijana wanaemualika wanauhakika kuwa atakubali kuitembelea Canada hivi karibuni, pengine hata kabla ya mwaka kuisha.

"Keshaalikwa sehemu nyingi pale Tanzania Bara na wala hajakataa. Hatudhanii kama atakataa mualiko wetu wa yeye kukutana na ndugu zake wakitanzania wanaoishi hapa Canada", alielezea mmoja wa vijana wanaomualika Dr. Shika kuenda huko Canada, tulivyozungumza nae kwa simu kutoka jiji la Toronto.

Tulivyomuuliza huyu kijana nini hasa kinachowafanya wamualike Dr. Shika huko Toronto na sio mtu mwengine yoyote yule kutoka Tanzania, alijibu,..." Kwanza, huyu bwana anajiamini. Ungelimuona wewe alivyokuwa akipandisha dau kwenye mnada basi ungelifahamu ninazungumza nini". 

"Pili, huyu bwana kaishi nje sana na kwahivyo matatizo ya huku nje atakuwa anayajua vizuri zaidi kuliko sisi wengine tuliokuja juzi juzi and therefore tunahisi tutafarajika sana kama baada ya chakula cha pamoja cha jioni cha Watanzania wote yeye atatupa advices zake juu ya vipi kuishi huku nje kwa mafanikio, kwasababu huku nje zipo changamoto nyingi sana na kama mtu hujakuwa na akili yako timamu basi huenda yakakukuta yaliyomkuta Firauni", alimalizia kijana.

Jitihada za kumpata Dr. Shika kutoka Dar Es Salaam ili tumuulize kama keshaupata mualiko huu kutoka Canada hazikuzaa matunda. Kila tunapompigia simu yake ya mkononi anatueleza kuwa yupo mkutanoni na kuwa itapendeza kama tutamtafuta baadae.

No comments :

Post a Comment