Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, December 27, 2017

Zanzibar Heroes dimbani Jumamosi hii!

Mashujaa wa Zanzibar watafunga mwaka mjini Pemba watakapocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Kombaini ya Pemba.Mechi hiyo itachezwa keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Gombani mjini Pemba.
Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein aliitaka timu hiyo kufika pia Pemba badala ya kuishia Unguja ikiwa ni baada ya kutinga hadi fainali ya Kombe la Chalenji na kushindwa na wenyeji Kenya.

Zanzibar Hereos ilionyesha soka safi la kuvutia katika michuano ya Kombe la Chalenji na kuwatoa kimasomaso Watanzania.

Meneja wa Kombaini ya Pemba, Steven Kapufi ambaye pia ni Meneja wa Hard Rock, amesema kikosi chao kipo tayari kabisa kwa mechi hiyo.

“Mechi itakuwa bure ili kutekeleza agizo la rais na tumejiandaa vizuri tayari kabisa kwa ajili ya mechi hiyo,” alisema.

Kombaini ya Pemba imepatikana kutoka katika timu mbalimbali kama Opec, Mwenge, Kizimbani, Hard Rock, Jamhuri, Shaba, Dogomoro na nyingine na itajumuisha wachezaji 18

Benchi la ufundi litakaloingoza timu hiyo ni kama ifuatavyo;
Kocha Mkuu Mzee Ali Abdallah - chipukizi
Kocha msaidizi Ussi Ally Juma - Hard Rock sack
Katibu Khamis hamad - ZFA  (Katibu msaidizi ZFA taifa)
Meneja Steven Kapufi-  Hard Rock SC
Daktari Hamidu Mapunda- Hard Rock SC
Daktari Msaidizi Saidi Ngonwe Hard Rock SC.

No comments :

Post a Comment