Alphayo Kidata anaweza kuwa ni mtu pekee katika Serikali ya Awamu ya tano ambaye ameweza kushika nafasi zaidi ya tatu muhimu katika muda wa miaka miwili.Kutoka Kamishna wa Mamlaka ya Mapato, kuwa kamishna kamili, kuwa Katibu Mkuu Ikulu hadi balozi, ikiwa ni mara yake ya nne kuteuliwa kushika nafasi mbalimbali muhimu tangu mwaka 2015.
Hiyo inatokana na uteuzi uliofanywa jana na Rais John Magufuli ambaye amempa Kidata wadhifa wa balozi anayesubiri kupangiwa kituo.
Taarifa iliyotolewa jana na mkuu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Gerson Msigwa inamnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akieleza kuwa Rais amemteua Kidata kuwa balozi kuanzia juzi.
Machi 2016, Rais Magufuli alimteua Kidata kuwa kaimu kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baadaye kumthibitisha kuwa Kamishna Mkuu.
Kabla ya uteuzi huo, Kidata alikuwa katibu mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nafasi aliyoishikilia tangu Agosti, 2013 alipoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo akitokea Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) ambako alikuwa naibu katibu mkuu.
Machi 23, 2017 aliteuliwa kuwa katibu mkuu Ikulu kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Peter Ilomo ambaye alistaafu. Amedumu kwa nafasi hiyo tangu wakati huo hadi jana alipoteuliwa kuwa balozi huku akisubiri kuapishwa na kupangiwa eneo lake la kazi.
Uteuzi wa Kidata kuongoza TRA ulitokana na mshikemshike ulioibuka katika mamlaka hiyo baada ya Novemba 27, 2015. Rais Magufuli kumsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade baada ya kuibuliwa kwa upotevu wa makontena 249 yenye thamani ya Sh80 bilioni katika Bandari ya Dar es Salaam pasipo TRA kuwa na kumbukumbu zozote.
Katika mabadiliko hayo, Rais alimteua Dk Philip Mpango kukaimu nafasi hiyo, lakini haikupita muda mrefu kwa kuwa Desemba 23, 2015, alimteua kuwa mbunge na kisha Waziri wa Fedha na Mipango na Kidata kukaimu nafasi hiyo.
Wazungumzia uteuzi
Wakizungumza na Mwananchi maoni yao kuhusu Kidata kuteuliwa nafasi tofauti ndani ya muda mfupi, baadhi ya waliohojiwa walisema hiyo inaonyesha imani kubwa na kuaminiwa kwake na Rais.
Wamesema Rais anaweza kuteua kulingana na historia nzuri ya utendaji wa anayemteua, lakini wakabainisha kwamba kuhamishwa kwake mara kwa mara kunaweza pia kumfanya mhusika ashindwe kuonyesha mabadiliko katika nafasi anayotoka kutokana na kutotumia muda mrefu.
Wakili Dk Onesmo Kyauke alisema jukumu la uteuzi huo, lipo mikononi mwa Rais na kusisitiza kwamba mtu anapoteuliwa, lazima atakuwa na upekee fulani katika kutimiza jukumu alilopangiwa katika kuleta mabadiliko.
Kuhusu kuhamishwa kwake mara kwa mara Dk Kyauke alisema pengine Rais ameona amemaliza kazi aliyomtuma na hivyo kumuhamishia sehemu nyingine.
Alisema kuna uhusiano wa karibu kati ya uzoefu na utendaji mzuri wa kazi, “Mfano mtu akiwa kamishna wa TRA kuna mambo lazima ajifunze ili aweze kutekeleza majukumu yake vyema, ukimhamisha anaweza kukosa focus (mwelekeo). Hata hivyo, hili si suala la kuhoji sana.”
Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Richard Mbunda alisema Katiba ya nchi inamuangalia zaidi Rais katika utendaji kuliko anaowateua, hivyo anaweza kuteua watendaji kulingana na anavyoona inafaa lengo likiwa ni kuwatumia kutimiza malengo yake. “Jambo hili linampa Rais uwezo wa kuteua apendavyo kulingana na utendaji kazi wa mtu ingawa kuhamishahamisha watendaji kunaweza kuwafanya wasifanye kile kinachotarajiwa kutokana na kukaa eneo moja kwa muda mfupi, hivyo kuonekana si watendaji wazuri na hata kuondolewa kabisa,” alisema.
/ Mwananchi.

No comments :
Post a Comment