Mgombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni (upande wa Mwenyekiti Prof. Lipumba anayetambuliwa na msajili wa vyama), Rajab Salum kwa tiketi ya CUF, amedai anauhakika chama chake kitashinda kwenye uchaguzi huu kwa zaidi ya 56% kutokana na utafiti alioufanya.
Akizungumza kwenye kampeni zinazoendelea kwenye jimbo la Kinondoni, Bw. Salum amesema kwamba anaamini kwamba wana CUF wameamua hivyo chama chake kitapata ushindi mnono ifikapo Februari 17.
Akizidi kuwaelezea wana Kinondoni kuhusu matumaini yake kwao, mgombea huyo amewaahidi kuwa endapo watampatia nafasi ya kwenda kuwawakilisha bungeni, kamwe hatoweza kuwasaliti na kununuliwa kama alivyofanya Mtulia (aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo) kisha kuhamia CCM na kwamba yeye anajua thamani ya wapiga kuwa wake.
“Kwa utafiti niliofanya ni kwamba mpaka sasa CUF tunao ushindi wa kushinda kwa asilimi 56 na niwaombe wana CUF kwamba tujitahidi mpaka siku ya Februari 17 tushinde kwa kishindo cha asilimia 80” amesema Salum.

No comments :
Post a Comment