Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, February 23, 2018

Diwani wa Chadema Auawa Morogoro!

Diwani wa Kata ya Namawala wilayani Kilombero, Godfrey Luena (CHADEMA) ameuawa usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.

Kwa mujibu wa mbunge wa Kilobero, Peter Lijualikali amesema.

Taarifa za awali zinasema kuwa usiku huu umeme ulikatika katika nyumba yake. Luena akatoka nje kutizama kama kuna shot maana nyumba za jirani zilikuwa na umeme. Alipozunguka nyuma ya nyumba yake kukagua umeme akalutana na kikosi cha watu wenye mapanga wakamkatakata hadi wakamtoa roho.

Ameandika Mbunge wa Mikumi @professorjaytz ameandika:

“Diwani wetu wa Chadema Kata ya Namwawala, Jimbo la MLIMBA (MOROGORO) GODFREY LUENA ameuawa usiku huu nyumbani kwake kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana, 😭😭😭R.I.P. LUENA.”

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limethibitisha kutokea kwa kifo hicho;

“Ni kweli diwani Luena ameuawa usiku wa huu, polisi wameshafika eneo la tukio wanaendelea na uchunguzi lakini ni mapema sana kutoa majibu kwamba kifo hicho kimesababishwa na nini, uchunguzi ukikamilika jeshi litatoa majibu,” alisema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Mtei.

No comments :

Post a Comment