Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, February 8, 2018

Gambia inajiunga upya katika jumuiya ya madola!

Takriban miaka mitano baada ya kujitoa katika jumuiya ya madola leo Gambia inajiunga upya.

Sherehe inafanyika leo Alhamisi katika makao makuu ya jumuiya hiyo mjini London kuidhinisha kurudi kwa nchi hiyo kama taifa mwanachama wa jumuiya ya madola.

Mnamo Februari 2017, rais mpya aliyechaguliwa Adama Barrow aliomba nafasi ya taifa lake kurudi kuwa mwanachama, na mwezi Desemba bunge nchini humo liliidhinisha ombi hilo la kurudi katika kundi hilo linalojumuisha mataifa yaliokuwa chini ya ukoloni wa Uingereza.

Gambia ilijiondoa katika jumuiya hiyo mnamo Octoba 2013.

Rais wa zamani Yahya Jammeh aliishutumu jumuiya hiyo kwa kuwa anachokitaja "taasisi ya ukoloni mambo leo".

Ilichukua wiki kadhaa za majadiliano na tishio la jeshi kuingilia kati kumlazimisha aachilie madaraka.

Nchi zilizorudi upya katika Jumuiya ya madola
Baada ya Afrika kusini, Pakistan na Fiji, sasa Gambia inakuwa nchi ya nne kurudi katika jumuiya ya madola.

Afrika kusini ilitangaza kujitoa katika jumuiya hiyo mnamo Mei mwaka 1961 baada ya kupitisha sheria ilioifanya nchi hiyo kuwa Jamhuri na kusitisha utawala wa malkia.

Ilijunga upya miaka 33 baadaye mnamo 1994 baada ya kumalizika kwa ubaguzi wa rangi nchini.

Mnamo 2008 Jumuiya ya madola ilikubali kuirudisha Pakistan mwaka mmoja baada ya kuusitishauwanachama wake kufuatia hatua ya kiongozi aliyekuwepo Pervez Musharaf kuidhinisha hali ya hatari na kuwazuia maelfu ya wanaharakati wa upinzani.

Gambia ilijiunga na jumuiya ya madola kwa mara ya kwanza mnamo 1965, muda mfupi tu baada ya kupata uhuru kutoka kwa Uingereza.

Ombi la Gabon mwaka jana kurudi katika jumuiya ya madola liliitikiwa na wengi, na sasa Gambia imerudi rasmi na imealikwa kuhudhuria mkutano wa viongozi wa serikali wa jumuiya ya madola huko London mwezi Aprili.

No comments :

Post a Comment