Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, February 7, 2018

HOW TO APPLY FOR THE e-PASSPORT OF TANZANIA!

HATUA ZA UJAZAJI FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI (MTANDAO).
Image result for IMAGES OF THE E-PASSPORT OF TANZANIA

1. INGIA KATIKA TOVUTI YA IDARA: www.immigration.go.tz KISHA NENDA KATIKA KITUFE CHA e-SERVICES
2. CHAGUA PASSPORT APPLICATION FORM;
3. CHAGUA OMBI JIPYA;
4. TIKI KIBOKSI KUKUBALIANA NA MAELEKEZO;
5. JAZA TAARIFA ZAKO KWA UKAMILIFU UKIFUATA MAELEKEZO NA MPANGILIO (FORMAT) KATIKA KILA KIPENGELE;

NB:
BAADA YA MWOMBAJI KUKAMILISHA KUJAZA TAARIFA ZAKE, ATAFAHAMISHWA YA KWAMBA USAJILI UMEKAMILIKA NA KUPATIWA NAMBA YA OMBI, AMBAYO NI MUHIMU AIANDIKE PEMBENI NA KUIHIFADHI KWA KUMBUKUMBU ZA BAADAE. KISHA ATAPEWA NAMBA YA KUMBUKUMBU YA MALIPO (CONTROL NUMBER) NA KUTAKIWA KWENDA KULIPIA MALIPO YA AWALI (ADVANCE FEE) YA TSH 20,000.

BAADA YA KUKAMILISHA USAJILI, NA KUPATIWA NAMBA YA OMBI NA NAMBA YA KUMBUKUMBU (CONTROL NUMBER), UKURASA UTAONEKANA KAMA IFUATAVYO:

UTARATIBU WA MALIPO YA ADA YA HUDUMA
YA PASIPOTI KWA KUTUMIA M-PESA/TIGOPESA

INGIA KWENYE MENU YA M-PESA/TIGOPESA (*150*00#/*150*01#)
1. Bonyeza Namba 4 (Lipa kwa M-Pesa) - VODA
2. Bonyeza Namba 4 (Kulipia Bili) - TIGO
Kisha Weka/Ingiza Namba ya Kampuni
3. Ingiza Namba (888999)
4. Ingiza kumbukumbu Namba(Ingiza Control Number inayoanzia na 99109…….)
5. Ingiza kiasi (kama ulivyo elekezwa Mfano: 20,000 nk.)
6. Utapata Maelezo kuwa unalipa pesa NMB
7. Ingiza Namba ya Siri
8. Hakiki
9. Utapata Meseji toka M-Pesa/Tigopesa kama muamala umekubalika;

Utapata meseji kutoka kwenye mfumo Namba 15200 
kama muamala umekubalika;

10. Mteja atatakiwa kurudi katika OMBI LINALOENDELEA:
11. Kisha ataingiza NAMBA YA OMBI/SIMU na NAMBA YA RISITI

Na hapo ataweza kupakua Fomu yake ya Maombi
Ataiwasilisha Fomu hiyo katika Ofisi ya Uhamiaji Makao makuu au Afisi Kuu Zanzibar 

UTARATIBU WA MALIPO YA ADA YA HUDUMA
YA PASIPOTI KWA KUTUMIA BENKI NMB/CRDB

1. Jaza fomu ya malipo ya kielectroniki;
2. Fuata maelekezo kama yanavyojieleza kwenye fomu;
3. Utapata meseji toka benki;
4. Utapata meseji toka kwenye mfumo Namba 15200 
kama muamala umekubalika.

1 comment :

  1. Kila ninavyo tuma ombi la pasi mpya linagoma

    ReplyDelete