Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan M. Mwinyi akizungumza na Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kusini na Mashariki mwa Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Canada, Bw. Marc-André Fredelte. Katika mazungumzo yao walijadili masuala ya ushirikiano katika masuala ya diplomasia, biashara na maendeleo. Bw. Fredelte yupo nchini kwa ziara ya kikazi.
Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mwinyi na Bw. Fredelte (hayupo pichani). Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvator Mbilinyi, Bw. Mustafa M. Ussi, Afisa Mambo ya Nje na Bi. Lilian Kimaro, Afisa Mambo ya Nje.
Mazungumzo yakiendelea
Balozi Mwinyi akiagana na Bw. Fredelte baada ya kumaliza mazungumzo yao
Picha ya pamoja
No comments :
Post a Comment