Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, April 27, 2018

Mkesha wa kifo cha Sokwe mkubwa Uganda kufanyika Ijumaa!

Ijumaa hii kutakuwa na mkesha wa kuomboelza kifo cha Sokwe mkubwa zaidi nchini Uganda aitwaye Zakayo ambaye amekufa akiwa na miaka 54.Mwaka 1964, Zakayo alikuwa na mwaka mmoja alipokutwa ametelekezwa magharibi mwa Uganda.Kituo cha elimu ya Hifadhi ya wanyamapori kimesema kuwa alitunzwa na wataalam na baadae alifikishwa kwenye hifadhi ya taifa akiwa na miaka 13.

Zakayo aliishi sehemu kubwa ya maisha yake katika hifadhi ya Entebbe, ingawa hapo kwa mujibu wa mamlaka nchini humo, alikuwa hatarini.Watalii walikuwa wanampa sigara na pombe ili awafurahishe.

Hifadhi hiyo kwa sasa imeboreshwa na Zakayo anayeitwa 'Babu' wa Sokwe wote nchini Uganda aliweza kuishi kwa raha

Wataalam wa uhifadhi wamemsifu Zakayo kwa kuwa balozi wa sokwe na wanyama wengine nchini Uganda.Wanasema wasifu wake ulisaidia kujipatia fedha kwa juhudi za uhifadhi na kuongeza idadi ya watalii

Mabaki ya Zakayo yatatunzwa kwa ajili ya utafiti na elimu.

No comments :

Post a Comment