Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza akikata keki ya sherehe ya Muungano na Mgeni Rasmi katika sherehe hiyo Naibu Gavana wa Jiji la Riyadh Dkt. Adel Al Jubail.
Ubalozi wa Tanzania nchini uliadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanzania mjini Riyadh kwa sherehe iliyojumuisha jumuiya wa wanadiplomasia, Watanzania na Wanadiaspora waishio nchini Saudi Arabia.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza(kulia) akizungumza jambo na Naibu Gavana wa Jiji la Riyadh Dkt. Adel Al Jubail wakati wa sherehe ya miaka 54 ya muungano wa Tanzania.
Baadhi ya Watanzania waishio Saudi Arabia wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanzania.
Picha ya pamoja na madaktari wa hisani wanaotoa huduma za afya Tanzania Bara na Zanzibar wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Baadhi ya wake wa Mabalozi wa Afrika waliohudhuria sherehe hizo kutoka kushoto Gabon, Gambia, Eritrea, Burkina Fasso, Tanzania, Cameroon, Ghana na Nigeria.
Baadhi ya wageni na waalikwa mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo.
No comments :
Post a Comment