Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, May 25, 2018

Seif aomba kuzungumza na Rais!


Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Zanzibar Maalim Seif, amemuomba Rais Dk. John Magufuli wakutane na wazungumze kwa lengo la kumaliza mgogoro wa Zanzibar na kudumisha Muungano.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Kipindi cha TUJADILIANE cha Union Tanzania Press Club (UTPC) jijini Mwanza, ambapo ameeleza utendaji kazi wa Mahakama za Zanzibar zinafuata amri ya viongozi wa serikali.

"Kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini ZEC kutangaza kurudia Uchaguzi wakati mshindi anajulikana ni kinyume cha taratibu na sheria hata katiba ya nchi yetu hairuhusu, mimi na wenzangu tulipata kazi ngumu kuhamasisha vijana waliokuwa wanataka kuingia barabarani waachane na vitendo hivyo," alifafanua.

Aidha amesema kuwa chama cha CUF Zanzibar wanashiriki uchaguzi kwa ajili ya mapambano kwani ndio chama kikuu cha upinzani Zanzibar, kwani waungwana na waombapo mazungumzo wapewe nafasi ili kujenga muungano wenye maendeleo kwa Taifa la Tanzania.

No comments :

Post a Comment