dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, July 25, 2018

Balozi Seif aridhishwa na ujenzi uwanja wa Mao Tse Tung!


Na. Thabit Madai                                                     
Makamo wa Pili wa Rais, Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema  ameridhishwa na kufurahishwa kwa  hatua  iliyofikia ya ujenzi wa uwanja wa michezo wa Mao Tse Tung uliopo mjini magharib Unguja.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara  fupi ya kukagua maendeleo ya ujenzi uwanja huo wa mchezo, alisema nimefurahishwa nakuridhishwa kwa hatua kubwa iliyofikia ya ujenzi wa kiwanja cha michezo ambapo inaleta matumaini ya kufufuka tena kwa michezo visiwani Zanzibar.

Amesema kukamilika kwa uwanja wa huo wa mchezo utafufua na kuleta matumaini kwa upande wa michezo na utachangia pua ongezeko la watalii nchini kutokana na na hatua kubwa zinazochukuliwa za kuimarisha michezo.

Aidha alisema serikali kuu itazingatia mipango maalaamu itakayo saidia kuimarika kwa upatikanaji wa wa vifaa vitakavyotumiwa na wanamichezo tofauti tofauti nchini.

Hata hivyo alitoa masikitiko yake kutokana na kupotea kwa michezo wa magongo ambao ulileta sifa kubwa zanzibar na Tanzania kwa ujumla kimataifa kutokana na umahiri wake kwa wakati huo.

Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Omar Hassan King alisema Uwanja wa Mao Tse Tung  utakaokuwa wa Kijamii zaidi tofauti na viwanja vyengine vya Michezo unatarajiwa kugharimu Dola za Kimarekani Milioni Tano sawa na shilingi za Kitanzania Bilioni 15.

Alisema Bilioni 11 sawa ya Yuan Milioni 29 zinatolewa na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China na Shilingi Bilioni 4 zitatolewa na Sewrikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya kuendeleza ujanei huo.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan King alisema mradi wa ujenzi wa  Uwanja huo unahusisha pia uimarishwaji wa Miundombinu  ikiwa ni pamoja na  ujengaji wa viwanja viwili vya Michezo wa Mpira wa Miguu ambavyo vyote vitawekewa Nyasi Bandia kwa lengo la kuwa na hadhi ya Kimataifa.

Alisema ipo sehemu itakayokuwa na Jengo la Michezo ya ndani { Indoor Games } kwa ajili ya Mpira wa Meza, Wavu, Pete, Majengo Mawili kwa matumizi ya Ofisi pamoja na kuwekwa zana  na Vifaa vya mazoezi vitakavyohimili hali zote za Hewa ukiwemo pia uzio utakaouzunguuka Uwanja wote.

Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo aliishukuru Wizara ya Kilimo, Mali Asili, Mifugo na Uvuvi kwa kusaidia Rasilmali ya Mchanga inayotumika zaidi kwenye ujenzi wa Mradi huo ambao ndio changamoto kubwa iliyokuwa ikiwasumbuwa Wakandarasi wa Ujenzi huo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo Zanzibar Bwana Pen Yang  aliithibitishia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwamba kazi ya ujenzi wa Uwanja wa Mao itaendelea kutekelezwa ili ikamilike katika kipindi kilichopangwa.

Bwana Pen Yang Uwanja wa Michezo wa Mao utaendelea kubakia katika Historia ya Uhusiano wa muda mrefu ulkiopo kati ya China na Zanzibar ulioanza mara tu baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.

Mwakilishi huyoi wa Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar alisema kwamba Kiongozi wa Taifa la China alitia saini Mkataba wa ushirikiano kati ya Nchi hiyo na Bara la Afrika ikihusishwa miradi tofauti ya maendeleo ikiwemo Sekta muhimu ya Michezo.

Ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Mau Tse Tung  uliopo Mtaa wa Mpirani Kikwajuni ulioanza mapema Mwezi Mei Mwaka 2017  unafanywa na Kampuni ya Kimataifa ya Zhengtai Group ya Nchini Jamuhuri ya Watu wa China unatarajiwa kukamilika rasmi ifikapoMwezi Oktoba Mwaka huu wa 2018.

No comments :

Post a Comment