VIONGOZI wa dini ya Kikristo wameeleza kusikitishwa na vitendo vya uchimbaji mchanga katika eneo la makaburi wanapozikia waumini wao la Mwanakwerekwe Unguja, kwa madai kwamba baadhi ya watu hulitumia kufanyia vitendo viovu vikiwamo vya uasherati na uvutaji bangi na dawa za kulevya.
Wakizungumza katika mkutano kati yao na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud, walisema kuwa watu hao pia wamekuwa wakifukua na kuviweka nje vifaa vya kuzikia.Askofu wa Kanisa la TAG Kariakoo Zanzibar, Dickson Kaganda alisema, inasikitisha kuona baadhi ya watu wakitumia sehemu waliolala wapendwa wao na kwamba wanawakosea waumini na Mwenyezi Mungu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, aliahidi kuchukua hatua ili kulinusuru eneo hilo kwa kuchangia matofali 200 kwa ajili ya kujenga ukuta.
Aidha, aliwataka viongozi wa dini kuendelea kuhubiri umoja, amani na ushirikiano miongoni mwa jamii ili kuharakisha maendeleo ya taifa na jamii kwa ujumla na kwamba iwapo watazingatia wajibu walionao kwa waumini wao, nchi itapiga hatua na kuepuka migogoro.
"Katika kutekeleza majukumu yenu, viongozi mnapaswa kushirikiana na viongozi wa serikali na kuhakikisha waumini wenu wanatimiza wajibu wao kikamilifu," alisema mkuu huyo wa mkoa.
Mahmoud aliwahakikishia viongozi hao kuwa serikali ya mkoa wake itaendelea kushirikiana na waumini wao ili kuwawezesha kufanya ibada zao kikamilifu na kusisitiza kwamba serikali za Tanzania zitaendelea kuwatumikia wananchi wake bila ya ubaguzi kwa kuwa Katiba zote mbili zinatambua uwepo wa dini za aina zote licha ya serikali kutokuwa na dini.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment