Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila anajadili juu ya kumchagua mgombea wa urais atakaepeperusha bendera ya muunagano katika uchaguzi ujao.
Wanachama wa muungano wa vyama vinavyomuunga mkono rais Kabila unaojulikana kama Common Front for Congo (FCC) wameitwa kwenye mkutano huo muhimu jioni hii huko Kingakati, makao ya rais yaliyopo nje ya jiji la Kinshasa.
Chanzo kingine, cha karibu na rais Kabila, kimefahamisha kuwa hii sio siri tena- ni kuhusu kumtaja mgombea wa urais atakaye uwakilisha muungano wa vyama vinavyo muunga mkono kabila.
Majina yanayovuma ni pamoja na waziri mkuu wa zamani Augustin Matata Ponyo, Mkuu wa shughuli za ikulu wa rais Kabila, Nehemie Mwilanya Wilondja na kiongozi wa Bunge la Kongo, Aubin Minaku.
Wagombea wana muda hadi kesho Jumatano saa12 na robo kwa saa za Afrika mashariki kuwasilisha makaratasi au fomu zao ushiriki katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 mwezi Desemba 23.
Uchaguzi huo wa rais ulioahirishwa mara mbili unaonekana kuwa muhimu ufanyike kwa ajili kupatikana utulivu kwa nchi hiyo inayokumbwa na migogoro. Rais Joseph Kabila, ambaye amekuwa madrakani tangu mwaka 2001, alipaswa kuachia madaraka mwishoni mwa 2016 wakati muhula wake ulipofikia ukomo wake. Kwa mujibu wa katiba rais anastahili kuhudumu kwa kipindi cha mihula miwili.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment