JANA August 08, 2018 Msanii Mkongwe wa Filamu Bongo, Mzee Majuto alifariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MHN) alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kutokana na umahiri wake katika sanaa ya maigizo kifo chake kimegusa wengi. Hiki ni kile walichoandika Diamond Platnumz, Wema Sepetu, Ali Kiba, Zamaradi, Ridhiwan Kikwete na Idriss Sultan kufuatia msiba huo.
Diamond Platnumz : May your Humble Soul Rest in Paradise KINGπ€΄...Will always Miss and Love youππ»
Idris Sultan: Kazi yangu ya mwisho kama photographer/graphic designer kabla ya kwenda BBA na ndo ilikuwa mara ya kwanza kukutana na King Majuto. Mara nyingi alikuwa haji anaagiza watu wanatuma picha ila hii alikuja.
Nakumbuka mzee aliniambia “We dogo una vituko sana ila kituko chako kikubwa kuliko vyote ni haujui unafurahisha kiasi gani, endelea kutokujua utashangazwa”... Sidhani kama mnajua kiasi gani unajiskia ukiambiwa kitu kama hicho na mfalme.
To this day nasikitika kuwa sikuwahi kumuambia alichonifanya ila naweza kumuahidi kuwa popote nitakapoenda nitahakikisha sifanyi kosa la kutokusema makubwa aliyotufanyia kama watoto wake kwenye comedy industry. FOREVER A KING inna lillahi. With respect I will never call myself KING na naomba isitokee nikaitwa pia.
Wema Sepetu : Alipangalo Allah... I wished to work with you baba angu... Ila Allah hakupanga... Kapumzike baba angu... Mungu Mkali jamani....πππ... Ila kama kuteseka tu umeteseka jamani.... RIP King...Zamari Mketema: “Muda umefika Baba Safiri Salama Kikubwa umeacha Alama kubwa kwenye Dunia na tasnia kwa ujumla Heshima yako itabaki milele PUMZIKA KWA AMANI”
Aunty Ezekiel: Rip Daddy…..πππ
Alikiba : Ewe Mwenyezi Mungu hakika Mzee Wetu Amri Bin Athuman (King Majuto) yuko katika dhima yako na kamba ya ujirani wako, basi mkinge na fitina ya kaburi na dhabu ya moto nawe ndiwe mstahiki wa utekelezaji na ukweli msamehe na umrehemu hakika Wewe ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu.AMIN.
Ridhiwan Kikwete : “Mzee Amri Athumani Baba , Rafiki na Mzee wangu Nakushukuru kwa Maisha Uliyoyaishi. MWENYEZI MUNGU Ana sababu katika Kuonyesha Upendo wake. Tunakushukuru kwa Kizazi Chako Pia…Alhaj Amri Majuto. Salamu za Pole ziende kwa Katibu Tawala Wangu wa Bagamoyo Ndg. Hamza Athumani na Nduguze wote. Tuko pamoja sana.Pumzika kwa Amani Baba Majuto”
No comments :
Post a Comment