dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 31, 2018

RC Mjini Magharibi ataja mikakati ya kumaliza msongamano eneo la Mji Mkongwe!

Mwenyekiti wa kikao cha usimamizi wa maendeleo ya mji na uhifadhi wa utamaduni Ayoub Mohammed Mahmoud amesema kuwa ataendeleza adhma ya serikali ya kuondoa tatizo la msongamano wa magari katika eneo la mjini mkongwe.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha Pili cha kamati ya usimamizi wa maendeleo ya mji na hifadhi ya utamaduni katika ukumbi wa mamlaka ya mji mkongwe amesema kuwa nia ya mpango huo ni kuhakikisha kuwa msongamano uliopo ndani ya mjini mgongwe unapatiwa ufumbuzi ili kuodosha usumbufu  kwa wananchi.Ayoub ambae pia ni mkuu wa mkoa wa mjini magharibi amesema kuwa taarifa ya kitaalamu juu ya mpango wa  huo itasaidia kuondoa  msongamano wa magari ndani ya mji mkongwe hatua itakayopeleka kuleta haiba inayohitajika ndani ya eneo hilo

Akiisoma ripoti ya kamati ya watalamu iliyoteuliwa na Mkuu wa mkoa  wa Mjini Magharibi  juu ya mapendezeko ya muongozo wa utekelezaji wa matumizi ya vyombo vya moto ndani ya mji mkongwe Mohamed Simba Hassan ameeleza kuwa ni vyema ikatolewa elimu ya kutosha kwa jamii  kuhusiana  na faida za kutunza mji mkongwe na matumizi sahihi ya barabara.

Aidha ameiomba taasisi ya  usimamizi wa mji mkongwe kukaa pamoja na taasisi zinazotoa huduma ya usafirishaji ,abiria na mizigo kutengeneza mfumo wa udhibiti na uingizaji wa vyombo vya moto katika eneo la mji  mkongwe .

Wakichangia ripoti ya kamati hiyo wajumbe hao wameeleza kuwa ni vyema taasisi  husika  kukaa na kutafakari juu ya suala zima la kuondosha msongamano wa magari katika maeneo ya mji mkongwe  na kuihamisha bandari  katika maeneo  hayo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa idara ya mipango miji na vijiji  ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya wataalamu   Dr mohd jabir mohd amesema kuwa  kuwepo kwa ufinyu wa barabara katika maeneo ya mji mkongwe kunapelekea foleni kubwa wakati meli zinaposhusha abiria .

Katika kikao hicho pamewasilishwa taarifa   mbili ikiwemo taarifa ya wataalamu juu ya njia za mji mkongwe  na taarifa ya utafiti  wa eneo la green corridor.

No comments :

Post a Comment