Baada ya Wabunge wa upinzani kutofika katika shughuli ya uzinduzi wa barabara ya juu 'Flyover' katika eneo la Tazara jijini Dar es salaam, CHADEMA wameibuka na kutoa sababu za Wabunge wake kutofika.
Wabunge wa upinzani kupitia CHADEMA jijini Dar es salaam ni John Mnyika wa Kibamba, Halima Mdee wa jimbo la Kawe pamoja na Saed Kubenea wa Ubungo.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, amesema, sababu zilizowafanya Wabunge hao kutokufika katika uzinduzi asubuhi ya leo ni kwa kuwa walikuwa na kesi katika Mahakama ya Kisutu.
“Tumemsikia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisema, leo Wabunge wa CHADEMA, walialikwa kwenye uUzinduzi huo na hawakufika, walikuwa Mahakamani wakati shughuli zikiendelea , hivyo wasingeweza kuwa Mahakamani na wakati huohuo wakahudhuria”, amesema Mrema.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment