KUFUATIA kauli ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Bashiru Ally kumtaka mbunge wa Lindi mjini ajisalimishe kwa sababu ya utoro bungeni na jimboni kwake. Chama Cha Wananchi-CUF Lindi mjini kimekitaka CCM kiwaombe radhi wananchi wa jimbo la Lindi mjini.
Wito huo kwa CCM umetolewa leo katika manispaa ya Lindi, na Mkurugenzi wa idara ya Vijana wa CUF Lindi mjini, Hamisi Sapanga alipozungumza na Muungwana akiitolea maoni kauli hiyo ya Dk Bashiru.
Sapanga ambae pia ni naibu mkurugenzi wataifa wa siasa na uhamasishaji amesema CCM kinatakiwa kuonesha uungwana kwa kuwaomba radhi wananchi wa Lindi kwa kitendo cha mbunge huyo anayetokana na chama hicho kutoonekana jimboni na bungeni.
Alisema kusimama majukwaani na kutaka ajitokeze hakutoshi na hakuna faida kwa wananchi wa Lindi badala yake kitendo hicho cha hasara kinachofanywa na mbunge Hassan Kaunje kinatumiwa kama mtaji wakupatia kura kwenye uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Liwale.
"CCM ilimuombea kura na kuwaaminisha watu wa Lindi kwamba Kaunje anafaa kuwa mbunge wao leo wakisimama majukwaani na kuwatangazia wananchi kwamba hafai hatuwaelewi,"alisema Sapanga.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment