WAKATI Kivuko cha MV. Nyerere kikiibuliwa na kuwa katika hali yake ya kawaida, imebainika kuwa jumla ya wanafunzi 33 walifariki dunia kwenye ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 228.
Pia imebainika kuwa miongoni mwa waliokufa ni watumishi sita wa serikali katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ambao miili yao ilitambuliwa na ndugu zao na mwanafunzi ambaye bado hajapatikana.Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Cornel Magembe, wanafunzi wa shule ya msingi waliokufa kwenye ajali hiyo walikuwa 20 wakati wale wa sekondari walikuwa 13, walimu wanne, mtumishi wa idara ya kilimo mmoja na mwingine wa idara ya afya ya Ukerewe.
Alisema wanafunzi wengi waliokufa walikuwa wamekwenda kununua vifaa vya shule katika gulio la Bugorora na kwamba huenda idadi yao ikaongezeka kwa kuwa utafutaji wa miili ya waliokufa bado unaendelea.
"Wanafunzi waliokufa ambao wako katika rekodi za shule za msingi katika wilaya yetu ya Ukerewe ni 20 na sekondari 13, ingawa bado kazi ya uopoaji miili inaendelea, hivyo hatujajua mpaka sasa tunaweza kufikia idadi ya wanafunzi wangapi," alisema.
"Kazi hiyo ikikamilika ndipo tutajua wanafunzi wangapi walikuwa ndani ya kivuko cha MV. Nyerere na tukipata taarifa zaidi za mwili wa mwanafunzi kuopolewa tutawataarifu," alisema Magembe.
Kwa mujibu wa Mratibu Elimu Kata ya Bwisya, Kilenge Mngata, katika sekondari ya Bwisya wanafunzi waliokufa katika ajali hiyo ni 11 na kati ya hao, mmoja bado hajapatikana na kwamba shule za msingi za Bwisya, Bugaramila na Katende nazo zimesema wanafunzi wao 20 walikuwamo kwenye kivuko hicho.
Aidha, jana majira ya saa 7:20 mchana ambayo ilikuwa siku ya tano tangu kazi hiyo ianze, kikosi cha ukoaji kilikinyanyua kivuko hicho hadi kukisimamisha wima.
Akizungumzia hatua hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, alisema hatua waliyofikia ni nzuri na ilifanywa na vikosi vya Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ, Polisi, Zimamoto na Uokoaji, Jeshi la Akiba (mgambo) Songoro Marine, Mkombozi Marine iliyotoa vifaa pamoja na feri kwa ajili ya kukinasua kivuko, Kampuni ya ORION 2 na GGM ambao nao walitoa vifaa.
"Kazi kubwa tuliyokuwa nayo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa iliyobaki ni kuondoa maji pamoja na mizigo ndani ya kivuko ili kiweze kuelea kisha kivutwe na kuondolewa majini," alisema.
Alisema wanataka kuhakikisha magari ambayo yalikuwamo ndani ya kivuko hicho nayo yanatolewa pamoja na miili ambayo itaonekana.
Naye Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, alisema michango iliyopatikana imefikia Sh. milioni 726.

No comments :
Post a Comment