KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe atakua mzungumzaji kwenye mkutano wa The World Transformed ulioandaliwa na vuguvugu la Momentum ukihusisha wanaharakati na wanazuoni mbalimbali duniani wenye mrengo wa kijamaa.
Zitto amepata nafasi hiyo baada ya kupata mualiko maalumu wa Kiongozi wa Chama kikuu cha Upinzani nchini Uingereza cha Labour, Jeremy Carbyn na atahudhuria pia mkutano mkuu wa chama hicho.
Taarifa iliyotolewa na ACT inasema kuwa Zitto atafanya mazungumzo pia na wabunge, watunga sera na watu mbalimbali kuhusu hali ya kidemokrasia na kisiasa nchini na kushauriana majawabu yatakayosaidia kurekebisha changamoto ambazo Tanzania inakabiliana nazo.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment