dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, October 1, 2018

Bwege akamatwa na Polisi, adaiwa kufanya mkutano wa hadhara bila kibali!


Mbunge wa jimbo la Kilwa kusini, Selemani Bungara (Bwege), madiwani watano na mkurugenzi wa idara ya habari,uenezi na siasa wa CUF wilaya ya Kilwa wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kufanya mkutano wa hadhara kinyume cha sheria.
Taarifa kutoka wilayani humu,ambazo zimethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai zimeeleza kwamba Bwege na wenzake, akiwemo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Abou Mjaka na mkurugenzi wa idara ya habari,uenezi na siasa wa Chama Cha Wananchi-CUF, Deo Chaurembo na madiwani wengine wanne wamekatwa leo katika mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Masoko.

Akieleza tukio hilo Ngubiagai amesema Bwege na wenzake wamekatwa leo saa 10.00 jioni wakiwa kwenye mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Kilwa Kivinje baada ya kukataa kutii zuio la jeshi la polisi ambalo lilimkataza asifanye mkutano huo.

Amesema jeshi la polisi lilizuzia kwa barua mkutano huo usifanyike kutokana na muombaji kushindwa kukidhi vigezo hata hivyo mbunge huyo aliamua kufanya huku akijua anapinga amri halali iliyotolewa na chombo halali cha dola.

Alisema kwa taarifa alizonazo kama mwenyekiti wa kamati na ulinzi na usalama ya wilaya hii,nikwamba bunge Bungara alitoa taarifa ya kufanya mkutano huo chini ya muda ambao alitakiwa atoe taarifa kwa mujibu wa sheria.Ambao ni saa 48 kabla ya muda wakufanyika mkutano husika.

Alisema kukamatwa kwake hakumaanishi kama serikali haitambui haki ya mbunge huyo kufanya mkutano kwenye jimbo lake.Bali jeshi la polisi linazingatia hali ya usalama katika eneo husika na wakati husika.Lakini pia usalama wake yeye mwenyewe.Hivyo linapozuia jambo lisifanyike linakuwa na nia njema.

"Mheshimwa mbunge na wenzake wameshindwa kuzingatia kwamba kuwepo kwa demokrasia hakuzuii utii wa sheria.Misingi mitano lazima iheshimiwe,ambayo ni demokrasia,utawala wa sheria,uwajibikaji,haki na wajibu na ushirikishaji.Yeye ameangalia demokrasia tu na kudharau utawala wa sheria,"alisema Ngubiagai.

No comments :

Post a Comment