dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 16, 2018

Lema ataka wakina Mengi kutoa tamko kuhusu kupotea kwa MO Dewji!


Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimeitaka Serikali kuruhusu wapelelezi wa kimataifa kuruhusiwa kuja kufanya uchunguzi wa tukio la kutekwa kwa Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji 'MO'.

Akizungumza na Wandishi wa habari, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless Lema amesema kwa mazingira ya tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara huyo ilikuwa ni lazima kwa Serikali kutilia mkazo suala la uchunguzi ikiwemo kuomba msaada wa kimataifa huku pia akisema sio jambo geni kwani hata Nchi zilizoendelea kama Marekani huomba msaada kwa Nchi marafiki.

Lema amesema kama MO ambaye anamiliki zaidi ya Trilioni 3 pamoja na Timu ya Soka ya Simba yenye mashabiki wengi nchini kwa aslimia 49 ilipaswa Serikali iwe seriaz kuanzia kwenye matamko na sio Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kukataza watu kujadili suala hilo.

" Kama MO ambaye ni Bilionea anatekwa katika Nchi yake mwenyewe basi niwahakikishie kuwa hakuna Mtanzania ambaye yupo salama, hebu jiulizeni kwani Waziri Mkuu hajatoa tamko lolote, jana Rais John Magufuli alikua anafanya mazungumzo na wakimbiza mwenge wa uhuru nilitegemea atoe tamko zito lakini hakufanya ivyo, hii ni jambo la hatari sana, " Amesema Lema.

Lema ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini amesema MO ametekwa karibu na yalipo makazi ya Makamu wa Rais, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba lakini pia karibu na makao makuu ya idara ya usalama wa Taifa jambo ambalo linaonesha ni jinsi gani kwa mtanzania wa hali ya chini ni rahisi kupotezwa zaidi.

" Kwa kitendo hiki nawahakikishia uchumi wa Nchi hii utadorora zaidi, watu wataondoa ofisi zao hapa na kwenda nchi jirani zenye uhakika wa amani, nitoe wito kwa taasisi za dini, wafanyabiashara, taasisi za wenye viwanda watoke hadharani wapige kelele maana alietekwa ni mwenzao.

" Ni wito wetu kwa akina Mengi na wafanyabiashara wa kihindi watoke wapige kelele na vile vyote tunavyovipigia kelele tuviweke hadharani na ili Serikali ijivue lawama basi waruhusu vyombo vya kimataifa na kama wakikataa basi watakua watuhumiwa namba moja," amesema Lema.

No comments :

Post a Comment