Mkazi mmoja wa kijiji cha Mnolela kilichopo katika halmashauri ya Wilaya ya Lindi ameuawa kwa kukatwakatwa mapanga na watu wasiojulikana wakati alipokuwa akimsaidia msichana aliyekuwa akibakwa porini.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 62 ametambulika kwa jina la Issa Selemani ameuawa wakati akimsaidia msichana huyo mwenye umri wa miaka 12 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano shule ya msingi Nikowela.
Wakizungumza na ITV, baadhi ya wanakijiji wameiomba serikali kusaidia juhudi za kumsaka mtu aliyefanya tukio hilo la mauaji huku wakilalamika kuwa hawana amani baada ya tukio hilo kwakuwa wanaogopa endapo atarudi tena na kuendeleza matukio hayo.
Mwili wa mzee Issa Selemani umezikwa leo, Novemba 18, saa saba mchana kijijini kwake Mnolela.
/ EATV
No comments :
Post a Comment