zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, November 25, 2018

LONDODN: MAALIM SEIF AENDELEA NA ZIARA YAKE NCHINI UINGEREZA!





THE CIVIC UNITED FRONT 


[CUF-CHAMA CHA WANANCHI] 


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


TAREHE: 25 NOVEMBA, 2018 


Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na ujumbe aliofuatana nao siku ya Ijumaa, Tarehe 23 Novemba, 2018 alianza rasmi ratiba ya ziara yake ya kikazi nchini Uingereza kwa kutembelea taasisi muhimu na kukutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa taasisi hizo.


Asubuhi ya siku hiyo, Maalim Seif akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na Katibu wake Mhe. Issa Kheir Hussein, walifika na kupokewa katika taasisi maarufu duniani inayoshughulikia masuala ya kimataifa, The Royal Institute for International Affairs, ambayo hujulikana kwa ufupi kwa jina la Chatham House iliyoko katika mtaa wa St. James's Square, katikati ya jiji la London.

Wakiwa Chatham House, Maalim Seif na ujumbe wake walikutana na Meneja Mwandamizi wa Idara ya Afrika katika Taasisi hiyo, Bibi Tighisti Amare na maofisa wengine wa taasisi hiyo.

Katika mazungumzo yake, Maalim Seif na ujumbe wake waliiarifu Taasisi hiyo hali ya mambo inavyoendelea Zanzibar na Tanzania kwa ujumla na hasa kuzorota kwa hali ya kisiasa na kidemokrasia, utawala wa sheria na haki za binadamu.

Baada ya kumaliza kikao chao cha Chatham House, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, na ujumbe aliofuatana nao waliendelea na ziara yao siku hiyo hiyo wakati wa mchana kwa kufika na kukaribishwa kwa heshima zote kwenye Makao Makuu ya Jumuiya ya Madola (The Commonwealth) yaliyopo Marlborough House, katika mtaa maarufu wa Pall Mall, jijini London.

Wakiwa Marlborough House, Maalim Seif akiwa na ujumbe aliofatana nao walipokewa na kukutana na kufanya mazungumzo ya kina na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, The Rt Hon. Patricia Scotland QC. Mazungumzo hayo yalijikita kwenye masuala ya hali ya kisiasa na mwelekeo wa demokrasia Zanzibar na Tanzania.

Jumuiya ya Madola ilikuwa ni mojawapo ya taasisi tano za kimataifa zilizokuwa na timu za Waangalizi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 ambapo timu yao iliongozwa na Rais Mstaafu wa Nigeria, Mhe. Goodluck Jonathan.

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Bwana Linford Andrew ambaye ni Mshauri Mkuu wa Kisiasa wa Jumuiya ya Madola.

Leo tarehe 25 November, 2018 mnamo saa11:00 jioni kwa saa za Uingereza, ambapo ni sawa na saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, Maalim Seif atazungumza na Wazanzibari na Watanzania wanaoishi nchini Uingereza.
Mkutano huo unatarajiwa kurushwa moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter.





No comments :

Post a Comment