Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 6, 2018

Maji kuanza kununuliwa kama umeme!


Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), inatarajia kuanza mpango wa kununua maji kwa kutumia Mita, ambapo hatua ya awali imeshakamilika na hatua ya pili inasubiri kutangazwa kwa zabuni.

Injinia Cyprian  Luhemeja ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA,  amesema mpango huo ulianza na hatua ya awali imeshakamilika japo kumekuwa na changamoto katika teknolojia kutokana na awali kutokuwepo kwa mfumo wa namna hiyo.

Aidha Injinia Luhemeja amesema walianza majaribio ya mfumo huo kwa kutumia MITA 10 za awali ambapo wamefanikiwa kwa asilimia kubwa, hivyo wanasubiri hatua ya pili ya kutangaza zabuni kwa ajili kushindana ili uweze kuanza kwa haraka.

Injinia Luhemeja amesema mamlaka hiyo inatarajia kuwarudishia maji wateja wake waliokatiwa kutokana na madeni ambapo kwa sasa wataweza kulipa madeni yao kidogo kidogo huku wakiendelea kutumia maji.

No comments :

Post a Comment