Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, November 29, 2018

MAMA ASHANGILIA MWANAWE KUUAWA!


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MTWARA, LUCAS MKONDYA, PICHA NA MTANDAO
KATIKA hali isiyo ya kawaida mwanamke aliyefahamika kwa jina la Ndilikuli Matupa, mkazi wa Kijiji cha Mkangaula, Masasi mkoani Mtwara, amefurahia kitendo cha mtoto wake aitwaye Abdallah Mahona kuchomwa moto hadi kufa.

Kijana huyo alichomwa moto hadi kufa na wananchi wenye hasira baada ya kufanya tukio la wizi na kukamatwa.

Mashuhuda walisema tukio hilo lilitokea juzi, majira ya saa 12 asubuhi, baada ya Mahona kudaiwa kuwajeruhi watu wawili katika harakati zake za kuiba, ndipo wananchi wenye hasira wakamtafuta na kumchoma moto mpaka kifo chake.

Akizungumzia tukio hilo, Ndilikuli Matupa, alisema hawezi kusikitika kutokana na tukio hilo, kwa sababu hata yeye binafsi alikuwa anaishi kwa hofu kubwa kwa vitisho kutoka kwa mtoto huyo.

Alisema mtoto huyo alikuwa akimkosesha raha hadi kusababisha alale nyumba za starehe na vilabu vya usiku na kukaa kwenye ngoma hadi usiku kuepuka kuuawa na mtoto huyo, kwa kuwa amekuwa akimtishia kumuua mara kwa mara.

 “Jamani sina masikitiko yoyote, nimeponea chupuchupu kuuawa na mtoto huyu mara nyingi. Nalazimika kulala vilabu vya usiku mtu mzima kama mimi na nilikuwa nawaacha wajukuu zangu mmoja wa kwake, mmoja wa kaka yangu, nakwenda kwenye disko wakati umri wangu si wa madisko, lakini nilifanya hayo yote kwa kumhofia marehemu,” alisema.

Naye Mnape Mohamed, ambaye ni miongoni mwa ndugu wa marehemu wanaoishi kijiji cha Mkangaula, alisema ndugu yake alikuwa  akijihusisha na vitendo vya wizi  na mara nyingi alikuwa akimpiga mama yake.

 “Mimi huyu marehemu ni ndugu yangu na matukio yake nayafahamu tangu siku za nyuma na hata juzi nilikuwa naye. Kwanza alifikia hatua anafanya mambo ya ajabu ajabu, mkatili kupita kawaida na mara kadhaa amekuwa akimpiga na kumdhalilisha mama yake mzazi,” alisema.

Mtendaji wa Kata ya Namalenga, Sijaona Binamu, alisema mara tu alipoanza kazi katika kata hiyo mwaka 2016, taarifa ya kwanza ya uhalifu aliyoipata ilimtuhumu  Abdallah kuwa alimuua mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2010.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya, aliiambia Nipashe kuwa ana taarifa za watu wawili kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali, baada ya kufanya tukio la wizi wilayani Masasi.

Alisema katika tukio hilo walikuwapo wezi watatu, ambao walikwenda kuvunja duka na kuiba na wakati wanakimbia wakiwa katika bodaboda, wawili kati yao walianguka na ndipo wananchi wakawaua.

No comments :

Post a Comment