Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, November 18, 2018

Rais Trump: Ripoti kamili ya mauaji ya Jamal Khashoggi kutolewa Novemba 20, 2018!


Rais wa Marekani Donald Trump amesema ripoti kamilifu inayohusu mauaji ya mwanahabari msaudia Jamal Khashoggi itakuwa imekamilika siku ya Jumanne Novemba 20, 2018.

Trump ambaye yupo katika ziara kwenye jimbo la California kufuatilia ajali ya moto iliyotokea kwenye jimbo hilo. Akijibu maswali ya wanahabari katika mji wa Malibu, alizungumzia taarifa iliyotolewa na shirika la ujasusi la Marekani (CIA) kwamba mrithi wa kiti cha enzi mwana mfalme Muhammed Bin Salman ndiye aliyetoa amri ya kuuawa kwa Khashoggi.

Alisema upembuzi wowote bado haujafanyika ni mapema sana kutoa taarifa ya aina hiyo na kwamba ripoti kamili haijakamilika.Aliongeza kwamba wiki ijayo kati ya Jumanne na Jumatano watampa taarifa, ripoti kamili ikiwa imekamilika.

No comments :

Post a Comment