Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 6, 2018

Serikali kuwaunganisha Wajasiriamali nje!

Serikali ya Zanzibar imeahidi kuwaunganisha wajasiriamali wa taasisi ya ‘Mwanamke chakarika’ na taasisi za nje, ili kujifunza maarifa mapya na ubunifu wa biashara unaokidhi viwango vya kimataifa.

Akizungumza katika kongamano la wajasiriamali lililofanyika kwenye ukumbi wa Idriss Abdulwakil Mjini Zanzibar, Waziri wa Biashara na Viwanda, Balozi Amina Salum Ali, alisema ili kuzalisha bidhaa zenye ubora, elimu ya ujasiriamali ni kitu cha msingi.Alisema serikali kupitia wizara anayoiongoza, itahakikisha bidhaa za wajasiriamali wa Zanzibar zinavuta soko la ndani na nje na kuwashawishi wananchi kupunguza mapenzi kwa bidhaa kutoka nchi jirani.

Waziri huyo, aliwataka wajasiriamali hao kutumia matamasha na maonyesho mbalimbali yanayofanyika nchini kutangaza bidhaa na shughuli zao kama njia moja wapo ya kuwafikia wateja.

“Masoko yanatafutwa kwa njia na mbinu mbalimbali, wizara yangu imepata jengo ndani ya Mji Mkongwe ambalo tutalitumia kuonyesha bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wetu ili kukuza uwezo wao wa uzalishaji na kuwapatia soko la bidhaa zao,” alisema.

Aidha, aliwataka vijana kubadili mawazo ya kusubiri ajira za serikali badala yake waanze kutumia maarifa na nguvu walizonazo kujiajiri katika nyanja mbali mbali ili kupambana na tatizo la ajira.

Naye Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Aisha Abdulkheir, alieleza kuwa lengo la kuwaunganisha wajasiriamali wanaozalisha bidhaa mbalimbali ni kuimarisha uwezo, ujuzi na kukuza mitaji yao.

“Muda wote tumekuwa tukiwashajihisha wanawake na vijana wa kike kushiriki katika uzalishaji mali ili kuepukana na utegemezi hivyo kongamano hili tumelifanya makusudi kuonyesha mafanikio ya baadhi yao kama njia mojawapo ya kuwahamasisha wengine kutumia mazingira yanayowazunguka kuzalisha fursa za ajira”, alisema Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake, Katibu wa taasisi hiyo, Abla Mohammed Bakari, alisema lengo la kuandaa kongamano hilo ni kuwahamasisha wanawake na vijana kujiajiri wenyewe badala ya kupoteza wakati wakisubiri ajira za Serikali ambazo ni chache.

No comments :

Post a Comment