Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mwita Waitara amesema kuwa serikali ina mpango wa kukarabati shule kongwe takribani 17.
Waitara amesema kuwa katika kukarabati shule hizo zimetengwa bilioni 17 ambapo ni sawa na bilioni moja kila shule.
"Mpango huu tunakarabati shule kongwe 17 zimetengwa takribani bilioni 17 maana yake maximum bilioni kila shule kwahiyo hiyo ni awamu ya pili huu ni mpango wa kwanza wa kuboresha elimu Tanzania," amesema Waitara akifanya mahojiano yake na Azam Tv.
July 28, 2018 Mwita alingo'ka kutoka kwenye Ubunge kwa tiketi ya Chadema na kujiunga na CCM.
No comments :
Post a Comment