Wanaume wapatao 10 ambao wanatuhumiwa kujihusisha na ushoga visiwani Zanzibar wamekamatwa na Jeshi la Polisi katika fukwe za Pongwe.
Taarifa za kukamatwa kwa watu hao, zimethibitishwa na Kamanda wa polisi wa Kusini Unguja, Suleiman Hassan ambapo amesema taratibu za kisheria na kiuchunguzi zitafuatwa.
Wiki iliyopita Kampeni ya kutokomeza ushoga ilitangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Paul Makonda, lakini hata hivyo baadae Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ilitoa tamko kuwa kampeni hiyo hawaifahamu na ni mtazamo wa mtu mmoja yaani Makonda.

No comments :
Post a Comment