Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 27, 2018

Zijue faida zitokanazo na ulaji wa matango kiafya!



Mwili wa binadamu ili uweze kuwa katika afya nzuri, unahitaji kuwa na virutubisho vya kutosha. Virutubisho hivi tunavipata katika vyakula, matunda na hata kupitia katika vinywaji mbalimbali tunaweza kupata vitu muhimu kwa ajili ya afya zetu.

Mpenzi msomaji, leo napenda kukufahamisha au kukukumbusha kuhusu faida zinazotokana na ulaji wa tunda hili maarufu sana, TANGO.

Miongoni mwa faida tunazozipata kwa kula matango ni hizi zifuatazo:
Kwanza kabisa, ulaji wa matango husaidia kuboresha kiwango cha maji ambayo huhitajika mwilini, hii ni kutokana na matango kuwa na kiwango kikubwa cha maji. Maji haya husaidia kuondoa taka mwili pamoja na sumu mbalimbali ambazo miili yetu huzipata kupitia vyakula, madawa na hata vinywaji.

Pili, husaidia kupunguza uzito wa mwili. Kutokana na matango kuwa na asili ya nyuzi nyuzi au fibres, humfanya mlaji ajisikie kushiba bila ya kuongeza vitu mwilini ambavyo husababisha mtu aongezeke uzito.

Tatu, hupunguza (hangovers),uchovu, mawengewenge pamoja na hali ya kujisikia vibaya kutokana na unywaji wa kilevi. Hii ni kutokana na kuwa na vitamini B na maji mengi ambapo, baada ya mtu kunywa kilevi na kisha akaja kula matango kabla ya kulala, itamfanya asubuhi asiamke huku akiwa na hangovers.

Nne, husaidia katika mmeng’enyo wa chakula, matatizo ya tumbo kama vile kuvimbiwa, tumbo kujaa gesi, vidonda vya tumbo na mengineyo hupungua kutokana na ulaji wa matango, husaidia kuondoa sumu tumboni na kurahisisha ufyonzwaji wa protein mwilini kutokana na uwepo wa kiwezeshaji cha kibaiolojia kinachoitwa, erepsin enzyme.

Tano, husaidia kuondoa msongo wa mawazo. Matango yana kiwango kikubwa cha vitamini B ambayo husaidia kuboresha utendaji kazi wa mishipa mbalimbali ya fahamu mwilini na hivyo kuondoa hatari ya mtu kuathirika na msongo wa mawazo unaosababishwa na maisha ya kila siku.

Sita, husaidia kuondoa hatari ya mtu kupata kansa. Yana kiwango kikubwa cha virutubisho vyenye asili ya mimea viitwavyo, lignans, ambavyo pamoja na vitamini c, husaidia kuondoa sumu mbalimbali na kuiboresha kinga ya mwili na hivyo kuepusha hatari ya mtu kupata kansa.

Saba, husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani. Kwa kukiweka kipande cha tango mdomoni kwa dakika kadhaa, huuwa bakteria mbalimbali wasababishao magonjwa mbalimbali ya kinywa na harufu mbaya mdomoni.

Mpenzi msomaji, tunakushukuru kwa kuendelea kuwa nasi katika page hii, tutazidi kukuletea dondoo mbalimbali za afya na usisite kuwasiliana nasi endapo utakuwa na maoni au jambo lolote la kutushirikisha juu ya afya zetu.

Tango lina virutubisho vingi na madini muhimu sana katika mwili wa binadamu. Kwa mujibu wa wataalamu wetu, miongoni mwa virutubisho na madini mengine yaliyomo;

 tango ni chanzo kizuri cha Kashiamu, Chuma, Phosforas, Potasiamu, Zinki, Kambalishe, Vitamini B complex, Vitamini C na Vitamin E.

FAIDA ZAKE MWILINI
Unaweza kusema kuwa kirutubisho cha ‘Potasiamu’ ndiyo chakula cha moyo, kwa sababu ‘potasiamu’ ndiyo inayouwezesha moyo kupiga mapigo yake ya kawaida na kuustawisha. Ulaji wa matunda na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha ‘potasiamu’ kama tango, ni muhimu sana kwa mtu mwenye matatizo ya moyo, presha ya kupanda na matatizo ya mapigo ya moyo.

Aidha, tango linaaminika kupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini (cholesterol), huimarisha misuli ya mwili na bila kusahau husaidia usagaji wa chakula tumboni hivyo kuondoa tatizo la ukosefu wa choo.

Virutubisho vilivyomo kwenye tango pia, hutoa afueni kwa mtu mwenye matatizo ya ini, kongosho, figo na matatizo katika kibofu cha mkojo.

Wataalamu wetu wanatueleza pia kuwa tango lina kirutubisho kinachojulikana kama ‘erepsin’ ambacho husaidia uzalishaji wa ‘amino acids’ ambazo ni muhimu kwa uzalishaji wa protini mwilini.

Vile vile, tango lina kiwango kingi cha Vitamin C, hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo yatokanayo na ukosefu wa Vitamin C, kama vile kutokwa na damu kwenye fizi, upungufu wa damu kwa watoto wachanga na kuota meno na mifupa vibaya.

KINGA YA SARATANI
Pengine faida kubwa kuliko zote unazoweza kuzipata kwa kula tango au juisi yake mara kwa mara ni kinga dhidi ya saratani za aina mbalimbali. Jambo hili linatokana na ukweli kwamba tango lina kiwango kikubwa cha ‘alkaline’ (uchachu). Kwa kawaida ‘seli’ za saratani ‘haziwezi kuishi’ kwemye mazingira yenye uchachu, hivyo tango kinga dhidi ya saratani.

DAWA YA MAGONJWA YA NGOZI
Tangu enzi na enzi, tango limekuwa likitumika katika masuala ya urembo wa ngozi, watu wengi hutumia tango kwa njia mbalimbali kutunza ngozi zao na kupendezesha sura zao. Hata baadhi ya vipodozi visivyo na madhara, hutengenezwa kutokana na tango.

Ulaji wa tango na unywaji wa juisi yake mara kwa mara, huondoa matatizo mengi ya ngozi yaliyomo ndani na nje ya mwili. Utakapotumia juisi ya tango kwa muda wa wiki mbili hadi tatu mfululizo, utakuwa na ngozi nyororo na yenye afya kushinda hata mtu anayetumia vipodozi.

JINSI YA KUANDAA JUISI YA TANGO
Ni rahisi sana, chukua tango lako moja au zaidi, lioshe vizuri na limenye, kisha katakata vipande tayari kwa kusaga, ama kwa mashine (blender/juicer) au kwa kutwanga kwenye kinu maalum, changanya na maji masafi kiasi ili kupata juisi kiasi cha glasi moja.

Unaweza kuweka sukari kiasi kidogo sana (kisizidi kijiko kimoja kwa glasi) ili kupata ladha au weka asali kijiko kidogo kimoja. Utapata matokeo mazuri na ya haraka kama ukinywa juisi yako kila siku asubuhi kabla ya kula kitu chochote.

Ili kutibu matatizo ya ngozi uliyonayo au magonjwa mengine kama tulivyoyaeleza hapo juu, kunywa juisi hiyo kwa muda wa wiki mbili hadi 4 mfululizo na angalia matokeo yake. Kwa ukuaji wa afya yako, weka mazoea ya kunywa japo mara mbili au tatu kwa wiki.

Vile vile, unaweza kujiwekea mazoea ya kula tango kwa njia mbalimbali kama vile kuchanganya na saladi, kachumbari au kutafuna lenyewe mara kwa mara, kwani faida zake mwilini ni nyingi.
/Muungwana.

No comments :

Post a Comment