Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, December 3, 2018

Balozi Kairuki awataka Watanzania wanaosoma China kujituma!


Watanzania  wanaosoma nchini Chini wametakiwa kuwa chachu ya maendeleo, ubunifu, kujituma na kujitolea kwa manufaa ya Taifa la Tanzania ikiwemo kuchangamkia fursa za kimaendeleo.

Hayo yalisemwa Desemba Mosi mwaka huu na Mgeni rasmi wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Jumuiya za Wanafunzi Watanzania Wanaosoma China- TASAFIC, Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki ambapo aliwataka pia kutanguliza uzalendo ili kuweza kujifunza kwa umakini.

Alisema watanzania wanaosoma nchini China juu ya masuala Tambuka haswa ya Kielimu, Kiutaratibu, Kinidhamu, Fursa mbalimbali na jukumu lao la kuwa chachu ya maendeleo, ubunifu, kujituma na kujitolea kwa manufaa ya Taifa letu.

Mkutano huu uliandaliwa na Shirikisho la Watanzania Wanaosoma China na Ubalozi wa Tanzania Nchini China Ulileta pamoja Watanzania wanaosoma katika miji mbalimbali China kama Beijing, Dalian, Fushun, Jilin, Jinzhou, Harbin, Henan, Nanjing, Tianjing na Wenyeji wa Mkutano Shenyang.

No comments :

Post a Comment