Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 4, 2018

Dkt. Shein aeleza mikakati inayochukuliwa ili kupambana na magonjwa ya miripuko!

Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza mikakati inayochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kupambana na maradhi mbali mbali yakiwemo ya miripuko ambapo yanapozuka huathiri watu wa rika zote wakiwemo watoto.

Dk. Shein aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo ya Watoto (UNICEF) nchini Tanzania Maniza Zaman aliyefuatana na Mkuu mpya wa Shirika hilo hapa Zanzibar Maha Damaj ambaye alifika kujitambulisha kwa Rais.Rais Dk. Shein alieleza kuwa miongoni mwa juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi sasa ni pamoja na kujenga mitaro mikubwa katika eneo la mji wa Zanzibar ambayo matokeo yake itaisadia kuondosha matuamo ya maji ambayo hatimae huleta maradhi ya miripuko na kulata athari kubwa kwa jamii.

Aliongeza kuwa katika kipindi kifupi ambacho bado mradi huo ujenzi wake unaendelea tayari mradi umeanza kuleta matumaini makubwa ambapo athari mbali mbali ambazo hapo siku za nyuma zilikuwa zikitokea zimepungua ikiwemo kutuama kwa maji pamoja na kuleta mafuriko.

Aidha, Rais Dk. Shein alieleza kuwa mbali ya jitihada hizo suala zima la elimu pamoja na kuendeleza Sera na mikakati ya Serikali katika kupambana na maradhi mbali mbali pamoja na kuimarisha ustawi wa akina mama na watoto zimekua zikichukuliwa.

Hata hivyo, Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kulipongeza Shirika la UNICEF kwa jitihada zake za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuhakikisha watoto wa Zanzibar wanapata haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na elimu, afya pamoja na huduma nyengine za kijamii.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alieleza kuwa kuwepo kwa Programu ya Pamoja ya Zanzibar” (ZIP), inayohusisha Mashirika tisa ya UN iliyozinduliwa hivi karibuni kutasaida katika kuleta mafanikio yaliokusudiwa kwa wananchi wa Zanzibar.

No comments :

Post a Comment