zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 23, 2018

KAULI NZITO YA BASATA KUHUSU DIAMOND , RAYVANNY, "WAONGO"


Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) nchini Tanzania limekanusha kuwafungulia wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny wanaotumikia adhabu ya kutojihusisha na sanaa kwa muda usiojulikana baada ya kufanya makosa mbalimbali ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Taarifa ya Naibu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Onesmo Kayanda iliyotolewa leo Jumamosi Desemba 22, 2018 imesema haijawaondolea adhabu hiyo na kuwakata wafuate maagizo waliyopewa ikiwamo kutofanya maonyesho nje ya nchi.
Jana, wasanii hao kupitia mtandao wa Instagram waliomba radhi kwa mamlaka mbalimbali nchini na jioni walionekana wakifanya mkutano na wanahabari nchini Kenya kutangaza maonyesho yao yanayoendelea.
"Ikumbukwe kuwa Desemba 18 tuliwafungia kutojihusisha na sanaa kwa kipindi kisichojulikana kwa kuimba kwa makusudi wimbo Mwanza tulioufungia kwa sababu za kimaadili,

"Baraza linasisitiza kuwa halijawafungulia wasanii hao, pia linawaonya kuacha kutoa taarifa za uongo kabla halijawachukulia hatua kali zaidi," imesema taarifa hiyo ya Kayanda.

Diamond na Rayvanny wameingia matatani wakituhumiwa kufanya makosa mbalimbali ikiwamo la kutumbuiza wimbo uliofungiwa, kufanya tamasha mkoani Mwanza bila kibali, kutoa lugha ya matusi jukwaani mkoani Mtwara na kutofuata taratibu za usajili wa matamasha.

No comments :

Post a Comment