Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 16, 2018

Maandamano nchini Ufaransa yasababisha watu 168 kukamatwa!



Katika maandamano yanayoendelea mjin Paris nchini Ufaransa, Jeshi la Polisi limewakamata waandamanaji 168.

Jeshi la Polisi limelazimika kutumia gesi ya kusababisha kutokwa na machozi kuwasambaratisha  kwa mara nyingine waandamanaji waliomiminika  mjini Paris.

Idadi ya waandamanji imeonekana kupungua ikilinganishwa na wiki zilizopita.

Maandamnao yamefanyika nchini Ufaransa  waandamanaji wakipinga kupanda kwa bei za mafuta na  ughali wa maisha.

Waandamanaji walikuwa wakiwarushia askari walinda usalama mawe na vilipuzi huku jeshi la Polisi likijibu kwa kufyatua  mabomu ya kusababisha kutokwa na machozi.

Majeruhi walipelekwa katika hospitali zilizokaribu na eneo kulikofanyika maandamano.

Vyombo vya habari nchini humu vimefahamisha kuwa watu 168 ndio waliokamatwa katika maandamano ya Jumamosi na kukumbusha kuwa watu 200 walikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika  maandamano mjini Paris.

No comments :

Post a Comment