Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesema kuwa japo kuwa amekuwa ni maarufu sana kutokana na kauli zake anazozitoa katika kazi, yeye si mtu wa mitandao.
RC Mwanri amesema kuwa yeye akiwa katika kazi hata yale maneno anayoyasema huwa ana tafsiri sheria na si vinginevyo.
"Matukio yale unapoyaona unajua mimi sio mtu wa mitandao na Instagram na nini na Jamii Forums, ni matokeo yanayotokea kwenye field kwa kawaida ile reaction yangu ninavyosema pale inatokana na uhalisia wa jambo linalojitokeza pale kama hilo unalosema la Sukuma ndani katika Mkoa wetu wa Tabora walikuwa wanaolewa wakiwa utotoni kwahiyo pale ninapoongea pale naitafsiri sheria," Mwanri ameiambia Dizzim Online.
Mkuu wa Mkoa huyo amepata umaarufu zaidi kutokana na maneno yake ya 'Sukuma ndani, Nyoosha Mkono jifanye kama unajikuna, Tutashuka nao jumla jumla, Tutapiga pasu pasu.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment