Muungano wa Baraza la Umoja wa Vyama vya Upinzani nchini wamelalalamikia muswada wa sheria ya mabadiliko ya vyama vya siasa nchini kwa kile walichokidai kuwa muswada huo umelenga kuwabana vijana hao.
Wakizungumza jana na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam vijana hao wametishia kuuchana muswada huo pindi utakapofikishwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa.
Aidha katika Mkutano vijana hao kutoka vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR - Mageuzi na CHAUMA waliingia kwenye mkutano huo kwa kile walichoashiria kuwa ni majonzi waliyokuwa nayo juu ya muswada huo."Leo hii sisi tumevaa nguo nyeusi, hatuoni 'future',sasa basi vijana tunataka umoja tunapinga ili tuendeleea kuwa wamoja, Taasisi zote za vijana nchi hii kwa mara ya kwanza tutatangaza safari na tutauchana muswada ukiwa unataka kuingia bungeni," alisema Likapo Bakari ambaye ni Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT wazalendo.
"Muswada unampa mamlaka msajili kutoka kuwa mlezi wa vyama vya siasa, hadi kuwa mdhibiti wa vyama vya siasa, hivyo basi baada ya kuutafakari kwa kina muswada huu, tumeona ndoto za vijana ziko hatarini kufa kabisa na hali ya vijana itakuwa mbaya zaidi kuliko hata ilivyo sasa, hatukubaliani nao hata kidogo," alisema Patric Ole Sosopi, Mwenyekiti BAVICHA.
Aidha Mwenyekiti wa JUVI-CUF taifa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mchinga mkoani Lindi, Hamidu Jabali, alisema kuwa mchakato wa vikao vya upembuzi wa muswada huo vinaendelea baada ya kila chama kutoa wajumbe wanne watakoingia katika timu waliyoiita ya ufundi ambapo watatoa tamko rasmi baada ya kumaliza mchakato huo.
No comments :
Post a Comment