zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 23, 2018

Mwanafunzi chuo cha mafunzo Pemba afariki akitengeneza Umeme!

Akithibisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoa wa Kaskazini Pemba, Sheikhan Mohammed Sheikhan, alimtaja marehemu huyo kuwa Hemed Suleima Seif (40) wa Taifu Wete.
Alifahamisha kabla ya kupatwa na ajali hiyo marehemu alikuwa akifundishwa ujuzi huo ili upate kumsaidia wakati atakapotoka chuoni.
Alieleza tukio hilo lilitokea saa 1:45 za asubuhi, wakati marehemu akiwa chini ya mwalimu wa fani hiyo wakijaribu kusawazisha kasoro za umeme katika jengo hilo.

Ni kweli tumepokea taarifa kutoka kwa wenzetu wa chuo cha mafunzo kuwa kuna mwanafunzi anaetambuliwa kwa jina la Hemed Suleiman, amefariki baada ya kupigwa na shoti ya umeme,” alisema.
Alieleza uchunguzi wa awali uliofanywa na madaktari wa hospitali ya Wete umebainisha kuwa marehemu aliathirika mwili mzima.
“Tayari maiti imekabidhiwa jamaa zake kwa mazishi na jeshi la polisi inatoa pole kwa wafiwa,” alisema.
Aliwaomba wananchi kuwa waangalifu wakati wanapokua katika harakati zao hasa katika suala zima la umeme.
Aidha aliwataka askari wa chuo cha mafunzo kutowatumia wanafunzi hao kwa shughuli kubwa kama hizo za kuunga umeme.
Marehemu ambae alikuwa na namba 87/2017 alifikishwa gerezani huko kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya.

No comments :

Post a Comment